Teknolojia: Nyenzo ya kuleta ufanisi katika manunuzi ya Umma
Picha kwa hisani ya supplychainstation.com Na: Yoswam Nyongera, Mtaalamu wa Manunuzi Matumizi ya teknolojia kwenye manunuzi katika nchi mbalimbali yamethibitika kuongeza ufanisi na kuleta suluhisho la baadhi ya chang- amoto katika manunuzi ya umma. Uzoefu umeonesha kwamba matumizi ya mifumo isiyo ya kielekroniki katika manunuzi, hata kama imean- daliwa na kutekelezwa vizuri, haileti tija, inahitaji rasilimali nyingi, muda mwingi wa usi- mamizi na inapunguza ushindani. Zipo teknolojia za aina nyingi zinazotumika katika manunuzi. Baadhi ya teknolojia hizo kwa lugha ya kiingereza ni E-Commerce, inayojumuisha e- procurement, e-tendering, e-pur- chasing, e-auction, e-sourcing, e- contracting na e-payment. Nyingine ni Supplier database, contract database, business inteligency, e-invoicing/e-payables na Enterprise Resource Planning systems. Ununuzi wa kisasa unahitaji matumizi ya mifumo na vifaa vya kielekroniki ili kwenda sambamba na mifumo ya kiu- tend...