Mzabuni zingatia haya unapojaza nyaraka za zabuni, wengi hukosa kwa vigezo hivi

Picha na gestorestenerife.org

Nyaraka za zabuni (Tender documents) ni mkusanyiko wa nyara-ka zinazoandaliwa na taasisi nunuzi kwa lengo la kuwaalika wazabuni wenye sifa za kushiriki katika mchakato wa zabuni ambapo hatimaye mmojawao hupatikana na kupewa tuzo ya mkataba.

Sehemu kubwa ya maelezo yaliyomo kwenye nyaraka za zabuni, huzingatia matakwa ya sheria ya manunuzi ya umma na kanuni zake. Aidha, kwa mujibu wa sheria ya manunuzi ya umma, taasisi nunuzi zinatakiwa kutumia nyaraka sanifu (standard tender documents) ambazo hutolewa na Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma.

Katika kufuatilia kwangu masuala hayo nimegundua kwa kiasi kikubwa wazabuni wamekuwa hawazingatii masharti yaliyowekwa kwenye kitabu cha nyaraka za zabuni na hivyo kuchangia kwa sehemu kubwa kukosa au kushindwa katika kinyang’anyiro cha zabuni hiyo.

Vitabu vyenye nyaraka za zabuni vimewekwa katika makundi tofauti kufuatana na aina ya ununuzi unaotakiwa kufanyika. Makundi ya ununuzi Manunuzi ya umma yamegawanyika katika makundi makuu yaVifaa/bidhaa, kazi za majenzi, huduma zisizohitaji ushauri wa kitaalam na Huduma za ushauri wa kitaalam. 

Vivyo hivyo, nyaraka sanifu za zabuni  zitolewazo na PPRA zimeandaliwa kulingana na makundi hayo. Sehemu kuu za kitabu cha zabuni ni:

I. Mwaliko wa kushiriki zabuni
(Invitation for Tenders)
II. Fomu ya zabuni (Form of ten- der)
III. Maelekezo ya jumla kwa waz- abuni (Instructions to tenderers)
IV. Maelekezo maalumu kwa
wazabuni (Tender data sheet)
V. Masharti ya jumla ya mkataba (General conditions of contract)
VI. Masharti maalumu ya mkata- ba (Special conditions of contract)
VII. Fomu ya usalama (Forms of security)

Hivyo, wazabuni wanaoshiriki michakato ya zabuni za umma, wanapaswa kuhakikisha kuwa wanajaza nyaraka hizi ipasavyo na kuomba miongozo kwenye taasisi nunuzi husika au PPRA ili wasipoteze nafasi ya kupata zabuni kwa kukosea kujaza nyaraka, licha ya kuwa na sifa na vigezo vya kutekeleza zabuni husika.

Chanzo: PPRA journal, Vol. X, 12th Edition


Comments

  1. kama nimesapplay vishaa na wakanisimamisha juuu ya bei wakati kwenye tenda mimi ndo nilikia chini ya wote hiii imekaaje?

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

Marekebisho Sheria ya Manunuzi ya Umma Yanavyochagiza Tanzania ya Viwanda

Hatua anazopaswa kuchukua mzabuni asiyeridhishwa na mchakato wa utoaji zabuni