Picha kwa hisani ya wisegeek Michakato ya zabuni inapaswa kufuata sheria na kanuni za manunuzi ya umma inayoitaka taaasisi ya serikali kuendesha michakato hiyo kwa uwazi, ushindani na usawa. Lakini endapo mzabuni aliyeshiriki mchakato wa zabuni iliyotangazwa na taasisi husika hataridhishwa na matokeo ya mchakato huo, anayo nafasi ya kukata rufaa ili kuipata haki yake. Sheria ya manunuzi ya umma inaelekeza kuwa mzabuni ambaye hakuridhiswa na mchakato, anapaswa kwanza kukata rufaa kwa mkuu wa taasisi husika (afisa masuuli) kwa kumuandikia barua ya malalamiko yake akieleza sababu za kutoridhishwa. Mkuu wa taasisi hiyo anapaswa kuyajibu malalamiko hayo ndani ya siku 14. Endapo mzabuni hakupata majibu ndani ya muda huo, ama hakuridhishwa tena na majibu yatakayotolewa dhidi ya malalamiko yake, anapaswa kukata rufaa kwenye Mamlaka ya Rufani za Zabuni (PPAA).
Comments
Post a Comment