Teknolojia: Nyenzo ya kuleta ufanisi katika manunuzi ya Umma
Picha kwa hisani ya supplychainstation.com |
Na: Yoswam Nyongera,
Mtaalamu wa Manunuzi
Matumizi ya teknolojia kwenye
manunuzi katika nchi mbalimbali yamethibitika kuongeza ufanisi na kuleta suluhisho
la baadhi ya chang- amoto katika manunuzi ya umma. Uzoefu umeonesha kwamba
matumizi ya mifumo isiyo ya kielekroniki
katika manunuzi, hata kama imean- daliwa na kutekelezwa vizuri, haileti tija,
inahitaji rasilimali nyingi, muda mwingi wa usi- mamizi na inapunguza
ushindani.
Zipo teknolojia za aina
nyingi zinazotumika katika manunuzi. Baadhi ya teknolojia hizo kwa lugha ya
kiingereza ni E-Commerce, inayojumuisha e- procurement, e-tendering, e-pur-
chasing, e-auction, e-sourcing, e- contracting na e-payment. Nyingine ni
Supplier database, contract database, business inteligency,
e-invoicing/e-payables na Enterprise Resource Planning systems.
Ununuzi wa kisasa
unahitaji matumizi ya mifumo na vifaa vya kielekroniki ili kwenda sambamba na
mifumo ya kiu- tendaji katika sekta nyingine. Mathalani, matumizi ya Teknolojia
ya Habari na Mawasiliano yanawezesha kampuni za ndani na nje ya nchi kushiriki
katika michakato ya zabuni bila kulazimika kusafiri kutoka eneo moja kwenda lingine.
Matumizi hayo
yanapotumika kikamilifu huongeza ufanisi katika utekelezaji wa misingi mikuu ya
manunuzi ya umma, ambayo ni pamoja na uwazi na haki, ushindani, fursa sawa katika
kushiriki zabuni za umma, matumizi sahihi ya fedha za umma na uadilifu.
Aidha, mifumo hii
ikitumika kikamilifu itaboresha, kuleta mabadiliko makubwa ya utendaji na
kupunguza malalamiko katika sekta ya ununuzi wa umma.
Baadhi ya faida za
kutumia mifumo na vifaa vya kielekroniki katika manunuzi ya umma ni:
a) Kuongeza uwazi katika manunuzi ya umma
kupitia dirisha moja.
b) Kuongeza ushiriki
katika zabuni za kitaifa na kimataifa na kutumia fursa hiyo.
c) Kupunguza gharama za manunuzi,
d) Kutunza vizuri
kumbukumbu za manunuzi na kuzipata taarifa kwa wakati, pale zinapohitajika. e)
Udhibiti wa matumizi yasiyo ya lazima (setting levels of authorization).
f)
Kuongeza ufanisi katika menejimenti ya mikataba.
g) Kupunguza vihatarishi vya manunuzi
(reduction of pro- curement risk). h) Kurahisisha na kuongeza uwezo katika
kaguzi, i) Kupunguza muda wa michakato ya zabuni na kupunguza makosa ya taarifa
au takwimu.
Michakato ya zabuni na
kupun- guza makosa ya taarifa au takwimu. Matumizi ya mifumo ya kielekro- niki
katika manunuzi ya umma yanaboresha ufanisi katika mae- neo yafuatayo:
Uwazi
na haki: Taarifa zinazo- husu matangazo ya zabuni zinapowekwa
kwenye mtandao ni rahisi kuonekana kwa watu wengi zaidi nje na ndani ya nchi na
hivyo kutoa fursa kwa waombaji wenye sifa kushiriki katika mchakato wa zabuni.
Aidha, taarifa za matokeo ya mchakato wa zabuni zinapo- tolewa kwa njia ya
mtandao inakuwa rahisi kwa waombaji walioshiriki mchakato na umma kwa jumla
kupata matokeo haraka na endapo kuna malalamiko yoy- ote yatawasilishwa na
kupatiwa majawabu kwa wakati.
Ushindani:
Washiriki wengi kwenye zabuni huleta ushindani wa bei na sifa na hivyo kusabisha
taasisi nunuzi kupata
vifaa na huduma zenye ubora kwa bei nafuu.
Matumizi
sahihi ya fedha za Umma: Kumekuwapo namalalamiko mengi ya
gharama kubwa katika manunuzi ya umma zinazochangiwa na bei kubwa za bidhaa na
huduma kuliko za soko, gharama za mchakato wa zabuni na usimamizi wa
utekelezaji wa mikataba. Matumizi sahihi ya
teknolojia yanasaidia
kupata taarifa za bei za soko na takwimu za upatikanaji wa bidhaa katika soko kwa
wakati muafaka (real-time arket information); taarifa hizo husaidia taasisi
nunuzi kuepuka manunuzi kwa bei kubwa ambazo haziwiani na bei za soko.
Aidha, bidhaa na huduma
zinazo- nunuliwa mara kwa mara (fre quently purchased commercial prod- ucts),
zinaweza kununuliwa kupitia utaratibu wa kielekroniki (online shopping) kutoka kwa
wazabuni wenye mikataba maalum (framework agreements) ili kupun- guza gharama
za michakato yamanunuzi. Mfumo huu unajulikana kama Dynamic Purchasing System ambapo
wazabuni wenye sifa hupewa mikataba kwa kipindi maalum bila kuweka bei, pia wafanyabiashara
wapya wenye sifa huruhusiwa kupewa mikataba wakati wowote wanapoomba.
Taasisi
nunuzi inapohitaji bidhaa, inawaalika kushindanisha bei zao(e-auction).
7md Store General Trading LLC
ReplyDelete7md Store General Trading LLC
milk thistle herbal supplement
mullein herbal supplement
nettle herbal supplement
parsley herbal supplement
passionflower herbal supplement