Kupata matangazo ya zabuni za umma, bofya HAPA ili uweze kupakua matoleo yote ya Tanzania Procurement Journal, jarida linaloandaliwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA).
Picha na gestorestenerife.org Nyaraka za zabuni (Tender documents) ni mkusanyiko wa nyara-ka zinazoandaliwa na taasisi nunuzi kwa lengo la kuwaalika wazabuni wenye sifa za kushiriki katika mchakato wa zabuni ambapo hatimaye mmojawao hupatikana na kupewa tuzo ya mkataba. Sehemu kubwa ya maelezo yaliyomo kwenye nyaraka za zabuni, huzingatia matakwa ya sheria ya manunuzi ya umma na kanuni zake. Aidha, kwa mujibu wa sheria ya manunuzi ya umma, taasisi nunuzi zinatakiwa kutumia nyaraka sanifu (standard tender documents) ambazo hutolewa na Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma. Katika kufuatilia kwangu masuala hayo nimegundua kwa kiasi kikubwa wazabuni wamekuwa hawazingatii masharti yaliyowekwa kwenye kitabu cha nyaraka za zabuni na hivyo kuchangia kwa sehemu kubwa kukosa au kushindwa katika kinyang’anyiro cha zabuni hiyo. Vitabu vyenye nyaraka za zabuni vimewekwa katika makundi tofauti kufuatana na aina ya ununuzi unaotakiwa kufanyika. Makundi ya ununuzi Manunuzi ya ...
Mwenyekiti wa Bodi ya PPRA, Balozi Marten Lumbanga (picha kwa hisani ya PPRA) Sheria ya manunuzi ya umma iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2016, ilitungwa mwaka 2011 lakini ilianza kutumika mwaka 2013 baada ya kukamilika kwa utungaji wa kanuni zake. Mwezi June mwaka jana, Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lilipitisha muswada wa marekebisho ya sheria hiyo na baadae Rais John Magufuli aliisaini na kuwa sheria kamili. Marekebisho yaliyofanyika baada ya kukusanya maoni ya wadau wa manunuzi ya umma yalilenga katika kupata thamani bora ya fedha kwenye manunuzi ya umma. Mabadiliko hayo yamechagiza ongezeko la fursa kwa kutoa upendeleo kwa makundi maalum, wazawa na viwanda vya ndani ya nchi. Hizi ni sehemu tatu kati ya nyingi zilizofanyiwa marekebisho kuboresha michakato ya manunuzi ya umma nchini. Kuzingatia bei za soko katika manunuzi: kifungu cha tisa cha sheria kimeitaka kila taasisi ya umma kuhakikisha kuwa ina taarifa ya bei za soko za bidhaa ...
Picha kwa hisani ya wisegeek Michakato ya zabuni inapaswa kufuata sheria na kanuni za manunuzi ya umma inayoitaka taaasisi ya serikali kuendesha michakato hiyo kwa uwazi, ushindani na usawa. Lakini endapo mzabuni aliyeshiriki mchakato wa zabuni iliyotangazwa na taasisi husika hataridhishwa na matokeo ya mchakato huo, anayo nafasi ya kukata rufaa ili kuipata haki yake. Sheria ya manunuzi ya umma inaelekeza kuwa mzabuni ambaye hakuridhiswa na mchakato, anapaswa kwanza kukata rufaa kwa mkuu wa taasisi husika (afisa masuuli) kwa kumuandikia barua ya malalamiko yake akieleza sababu za kutoridhishwa. Mkuu wa taasisi hiyo anapaswa kuyajibu malalamiko hayo ndani ya siku 14. Endapo mzabuni hakupata majibu ndani ya muda huo, ama hakuridhishwa tena na majibu yatakayotolewa dhidi ya malalamiko yake, anapaswa kukata rufaa kwenye Mamlaka ya Rufani za Zabuni (PPAA).
kupata matangazo ya zabuni
ReplyDelete