Hatua anazopaswa kuchukua mzabuni asiyeridhishwa na mchakato wa utoaji zabuni


Picha kwa hisani ya wisegeek

Michakato ya zabuni inapaswa kufuata sheria na kanuni za manunuzi ya umma inayoitaka taaasisi ya serikali kuendesha michakato hiyo kwa uwazi, ushindani na usawa.
Lakini endapo mzabuni aliyeshiriki mchakato wa zabuni iliyotangazwa na taasisi husika hataridhishwa na matokeo ya mchakato huo, anayo nafasi ya kukata rufaa ili kuipata haki yake.

Sheria ya manunuzi ya umma inaelekeza kuwa mzabuni ambaye hakuridhiswa na mchakato, anapaswa kwanza kukata rufaa kwa mkuu wa taasisi husika (afisa masuuli) kwa kumuandikia barua ya malalamiko yake akieleza sababu za kutoridhishwa. Mkuu wa taasisi hiyo anapaswa kuyajibu malalamiko hayo ndani ya siku 14.
Endapo mzabuni hakupata majibu ndani ya muda huo, ama hakuridhishwa tena na majibu yatakayotolewa dhidi ya malalamiko yake, anapaswa kukata rufaa kwenye Mamlaka ya Rufani za Zabuni (PPAA).

PPA itapitia malalamiko yake na kusikiliza pande zote mbili (upande wa taasisi iliyoendeshs mchakato wa zabuni pamoja na mzabuni) na mwisho itatoa maamuzi kwa mujibu wa sheria. 
Hata hivyo, endapo mzabuni hataridhishwa pia na maamuzi hayo ya PPAA anayo nafasi ya mwisho ya kukata rufaa kwenda Mahakama Kuu.


Utaratibu huo uliowekwa kisheria ukifuatwa, mzabuni atapata haki yake kwa mujibu wa sheria badala ya kuishia kulalamika kwenye vyombo vya habari na kuitaka Serikali imchukulie hatua mkuu wa taasisi husika, kwa lugha iliyozoeleka sasa ‘kumtumbua’. 

Comments

Popular posts from this blog

Mzabuni zingatia haya unapojaza nyaraka za zabuni, wengi hukosa kwa vigezo hivi

Marekebisho Sheria ya Manunuzi ya Umma Yanavyochagiza Tanzania ya Viwanda