Marekebisho Sheria ya Manunuzi ya Umma Yanavyochagiza Tanzania ya Viwanda
Mwenyekiti wa Bodi ya PPRA, Balozi Marten Lumbanga (picha kwa hisani ya PPRA) |
Sheria ya
manunuzi ya umma iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2016,
ilitungwa mwaka 2011 lakini ilianza kutumika mwaka 2013 baada
ya kukamilika kwa utungaji wa kanuni zake.
Mwezi June mwaka
jana, Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lilipitisha muswada wa
marekebisho ya sheria hiyo na baadae Rais John Magufuli aliisaini na kuwa
sheria kamili.
Marekebisho yaliyofanyika baada ya
kukusanya maoni ya wadau wa manunuzi ya umma yalilenga katika kupata thamani
bora ya fedha kwenye manunuzi ya umma. Mabadiliko hayo yamechagiza ongezeko la
fursa kwa kutoa upendeleo kwa makundi maalum, wazawa na viwanda vya ndani ya
nchi.
Hizi ni sehemu tatu kati ya nyingi
zilizofanyiwa marekebisho kuboresha michakato ya manunuzi ya umma nchini.
Kuzingatia bei za soko katika manunuzi: kifungu cha tisa
cha sheria kimeitaka kila taasisi ya umma kuhakikisha kuwa ina taarifa ya bei
za soko za bidhaa nahuduma inayotumika mara kwa mara ili bei ya bidhaa na
huduma zitakazonunuliwa, zilingane na za soko. Aidha, GPSA haitapanga bei
kwenye mikataba (framework agreements).
Fursa kwa makundi maalum:
Kifungu cha 64
2(c) kimeweka sharti la kutoa upendeleo katika zabuni
mbalimbali, hasa
kwa makundi maalumu kama vile wanawake, vijana, wazee na watu wenye mahitaji maalumu,
ili waweze kufanya biashara na taasisi za umma.
Kukuza na kuendeleza viwanda vya ndani:
Sheria imetoa
kipaumbele cha kukuza na kuendeleza viwanda vinavyozalisha malighafi
nchini ili kukuza
uchumi na kutoa motisha kwa wamiliki wa viwanda kuongeza uzalishaji.
Chanzo: Tanzania
Procurement Journal, Vol. X, 9th Edition
Comments
Post a Comment