Posts

Showing posts from June, 2017

Teknolojia: Nyenzo ya kuleta ufanisi katika manunuzi ya Umma

Image
Picha kwa hisani ya supplychainstation.com Na:  Yoswam Nyongera, Mtaalamu wa Manunuzi Matumizi ya teknolojia kwenye manunuzi katika nchi mbalimbali yamethibitika kuongeza ufanisi na kuleta suluhisho la baadhi ya chang- amoto katika manunuzi ya umma. Uzoefu umeonesha kwamba matumizi ya mifumo  isiyo ya kielekroniki katika manunuzi, hata kama imean- daliwa na kutekelezwa vizuri, haileti tija, inahitaji rasilimali nyingi, muda mwingi wa usi- mamizi na inapunguza ushindani. Zipo teknolojia za aina nyingi zinazotumika katika manunuzi. Baadhi ya teknolojia hizo kwa lugha ya kiingereza ni E-Commerce, inayojumuisha e- procurement, e-tendering, e-pur- chasing, e-auction, e-sourcing, e- contracting na e-payment. Nyingine ni Supplier database, contract database, business inteligency, e-invoicing/e-payables na Enterprise Resource Planning systems. Ununuzi wa kisasa unahitaji matumizi ya mifumo na vifaa vya kielekroniki ili kwenda sambamba na mifumo ya kiu- tend...

Mzabuni zingatia haya unapojaza nyaraka za zabuni, wengi hukosa kwa vigezo hivi

Image
Picha na gestorestenerife.org Nyaraka za zabuni (Tender documents) ni mkusanyiko wa nyara-ka zinazoandaliwa na taasisi nunuzi kwa lengo la kuwaalika wazabuni wenye sifa za kushiriki katika mchakato wa zabuni ambapo hatimaye mmojawao hupatikana na kupewa tuzo ya mkataba. Sehemu kubwa ya maelezo yaliyomo kwenye nyaraka za zabuni, huzingatia matakwa ya sheria ya manunuzi ya umma na kanuni zake. Aidha, kwa mujibu wa sheria ya manunuzi ya umma, taasisi nunuzi zinatakiwa kutumia nyaraka sanifu (standard tender documents) ambazo hutolewa na Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma. Katika kufuatilia kwangu masuala hayo nimegundua kwa kiasi kikubwa wazabuni wamekuwa hawazingatii masharti yaliyowekwa kwenye kitabu cha nyaraka za zabuni na hivyo kuchangia kwa sehemu kubwa kukosa au kushindwa katika kinyang’anyiro cha zabuni hiyo. Vitabu vyenye nyaraka za zabuni vimewekwa katika makundi tofauti kufuatana na aina ya ununuzi unaotakiwa kufanyika. Makundi ya ununuzi Manunuzi ya ...

Mapendekezo ya ripoti ya CAG kwenye zabuni za umma yachagize uwajibikaji

Image
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Mussa Juma Assad (Photo by Mwananchi online) Na: Nelson Kessy (Afisa Mahusiano, PPRA) Katika toleo la wiki iliyopita tulichapisha makala iliyokuwa inatoa changamoto kwa wataalam wa manunuzi katika serikali za m mitaa kujifunza kutoka kwenye ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG). Aidha, makala hiyo ilijikita zaidi katika mamlaka za serikali za mitaa 171, na yalionesha kuwa taasisi 50 zilikiuka sheria ya manunuzi ya umma katika michakato ya manunuzi. Makala ya leo itaongelea umuhimu wa kuzingatia mapendekezo yaliyotolewa na CAG katika ripoti yake hiyo ya mwaka wa fedha 2015/16. Ripoti hiyo imeweka wazi kuwa ni vyema taasisi zilizokaguliwa kuhakikisha zinazingatia matakwa ya sheria ya manunuzi, hasa katika eneo la uandaaji na utekelezaji wa mpango wa mwaka wa manunuzi, ambapo zinapaswa kuwasilisha kwa  Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA) mipango ya manunuzi ya mwaka na ripoti za utekelezaji ...