MAKALA: Waandishi wa habari ongezeni ‘wino’ kwenye manunuzi ya umma
Picha na planetminecraft.com Na: Joseph Muhozi Kwanza niwapongeze waandishi wa habari nchini kwa kazi nzuri wanayoifanya kuwahabarisha wananchi kuhusu mambo muhimu yenye maslahi ya umma katika sekta mbalimbali nchini. Nikiwa kama sehemu ya wana taaluma wa habari, natambua changamoto ziliko mbele yetu, lakini bado waandishi wengi wamekuwa wakitanguliza mbele maslahi ya umma. Tumekuwa tukishuhudia kazi nzuri ya vyombo vya habari kwa ujumla wao sio tu katika kuuhabarisha umma, bali pia kuelimisha umma kadiri iwezekanavyo kwa kufanya uchambuzi rahisi kuhusu bajeti ya serikali punde inaposomwa bungeni. Pia, kazi nzuri kama hiyo kwa kiwango cha kuridhisha hufanywa pale inapotoka ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), na pale inapotoka ripoti ya ukaguzi unaofanywa na Mamlaka ya Manunuzi ya Umma (PPRA). Hata hivyo, kwa kuzingatia kwamba wanahabari wanalo jukumu la kitaaluma la kuwajibika kwa umma na kuwa walinzi makini wa maslahi ya umma dhidi...