Posts

Showing posts from April, 2017

Marekebisho Sheria ya Manunuzi ya Umma Yanavyochagiza Tanzania ya Viwanda

Image
Mwenyekiti wa Bodi ya PPRA, Balozi Marten Lumbanga (picha kwa hisani ya PPRA) Sheria ya manunuzi ya umma iliyofanyiwa marekebisho  mwaka 2016, ilitungwa mwaka 2011 lakini ilianza kutumika  mwaka 2013 baada ya kukamilika kwa utungaji wa kanuni zake. Mwezi June mwaka jana, Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lilipitisha muswada wa marekebisho ya sheria hiyo na baadae Rais John Magufuli aliisaini na kuwa sheria kamili. Marekebisho yaliyofanyika baada ya kukusanya maoni ya wadau wa manunuzi ya umma yalilenga katika kupata thamani bora ya fedha kwenye manunuzi ya umma. Mabadiliko hayo yamechagiza ongezeko la fursa kwa kutoa upendeleo kwa makundi maalum, wazawa na viwanda vya ndani ya nchi. Hizi ni sehemu tatu kati ya nyingi zilizofanyiwa marekebisho kuboresha michakato ya manunuzi ya umma nchini.  Kuzingatia bei za soko katika manunuzi: kifungu cha tisa cha sheria kimeitaka kila taasisi ya umma kuhakikisha kuwa ina taarifa ya bei za soko za bidhaa ...